Nendeze ni kati ya filamu ya kitanzania inayofanya vizuri katika tasnia hii ya filam ikiwa ni muendelezo wa filam ya mwali wa kizaramo.
Sio siri penye sifa acha wapewe sifa kiukweli wamejitahidi kwenye uandaji wa filam hii haswa kwa upande wa mapigano (action) ukizingatia ni wasanii wachanga ambao ndio kwanza wanaanza lakini wamefanya mambo mazuri sana kwani hata katika upangaji wa ngumi wamepanga vizuri halikadhalika pia washiriki wameshiriki vyema kwa inaonesha ni wazi kuwa walifanyia mazoezi ya kutosha sana tofauti na tulizoea kuona mambo hayo yakifanywa na wasanii wakubwa kama kina Bad Boy, na Seba.
Tofauti na wasanii wengine wamezoea kushirikisha wasanii wakubwa ili kutoka kisanaa, lakini ni kitu cha kufurahisha sana kuona kuwa kuna vipaji vikubwa nyuma ya pazia mbali na kina Vicent Kigosi, Jacob Stephen, Hemedi Suleiman ambao ndio wamezoeleka kama mtu ukitaka kuuza filam zao kazi yako na kama tukiendelea kutoa kazi nzuri kama hizi basi tutafika mbali, ingawaje ni filamu ambazo hazina soko kubwa sana kwasababu bado ni wasanii wachanga.
Pamoja na hayo bado kuna kasumba ya kuwa ili mtu ujulikane ama uonekane kuwa ni ni jambazi ama una mabavu ni lazima atavaa koti kubwa na anakuwa anatembea kwa kujitanua sana hata sijui ni kwanini na ndo tumeshazoea kwanini wasiwe tu wanaonekana kawaida kwani ili mtu kuwa jambazi si lazima utumie nguvu kwani hata akili tu inatosha lakini hilo ni swala gumu kwa watanzania, ingekuwa ni bora zaidi kama wangejaribu kucheza filamu ambazo wanatumia akili zaidi kwani filam nyingi za kibongo mtu ukitizama unakuwa unajua kabisa mwisho wake utakuaje na story nyingi zinakuwa zikijirudia.
Stori inamuhusu Nendeze(Latifa Shabani) ambae alitokea kumpenda kijana Mashaka ( na kukataa kuolewa na kijana wa kitajili Mr.Karan (Hashim Rajab Dituth) ambae alipendekezwa na wazazi wake kitendo amnbacho kinachosababisha vita na familia kumtenga kwa kuwa alikiuka matakwa ya familia yake,pamoja na hayo Mudi(Mohamed Salum) ambae ni kaka wa Nendeze alikuwa akipinga mapenzi ya mashaka na Nendeze hakuridhika kuwaona wakiwa pamoja hivyo kuchoma nyumba yao moto, lakini Nendeze na Mashaka walifanikiwa kujiokoa kwenye moto huo na kwenda kujificha porini ndipo wanakijiji walipoamua kujiunga na kuwatafuta na ndipo vita kati ya kikosi cha Mudi na Wanakijiji lakini mpaka mwisho wa siku walifanikiwa kushinda na kuendelea kuishi vizuri na familia zao.
Aina ya Filam:Migogoro ya Kifamilia, Mapigano
washiriki: Mohamed Salum, Latifa Shabani, Halima Hashim, Hashim Rajab Dituth.
Tuesday, October 28, 2014
Monday, October 20, 2014
Sunday, October 19, 2014
MUZIKI WA BONGO UPO JUU KULIKO FILAMU
Ni wazi kuwa soko la muziki linakuwa kwa kasi sana kuliko soko la filamu kwa upande wa Tanzania kwani hata katika upande wa ubora pia wapo juu kuliko upande wa filamu.
Sasa sijui ni ubahili wa wandaaji ama inakuaje, na kama ni ubahili hii kasumba itaisha lini wakati huu ndo muda wa kutambulisha soko letu kitaifa kutokana na utandawazi kama upande wa muziki wanavyofanya sio siri wasanii wa muziki wanajitahidi katika swala la kuitambulisha Tanzania kimataifa tofauti na upande wa filamu maana tangu Kanumba afariki sijawahi ona filamu iliyoigizwa kwa kushirikisha wasanii wa nje kama alivyokuwa akifanya marehemu Kanumba (The Great)
Tulizani kuwa kifo chake ndo kingekuwa ni changamoto kwa waigizaji wakubwa kama Vicent Kigosi (Ray) kuendeleza pale alipoachia marehemu lakini matokeo yake filamu nyingi zinakuwa katika mfumo wa vichekesho ambapo ndipo wasanii wengi wanapokimbilia siku izi kwasababu hazina garama sana, kwa mtindo huu tutaendelea kweli?
Sio siri filamu za kitanzania huwa zinatia uvivu sana kutizama hasa kwa wale wenye elimu ya juu tena ndo huwaga hawataki hata kuzisikia kabisa, na ndio maana hatuendelei kwasababu sisi wenyewe kama watanzania tunashindwa kuchangia soko hili la filamu kwasababu hazina ubora, kwanini tusitumie pesa nyingi katika kutengeneza filamu ili badae ilete faida zaidi? kwani mataifa mengine wameweza wananini mpaka watanzania tushinde?
Waandaji achene ubahili ili kutengeneza kazi iliyo bora kama wasanii wakubwa wanavyofanya kama Diamond, Linah na Ommy Dimpoz.

Tuesday, September 30, 2014
BONGO MOVIE KUFIKIA NGAZI YA HOLLYWOOD HATUA BADO NI NDEFU SANA
"We are 4" (Tupo wanne) ni kati ya filamu mpya zilizotoka ndani ya mwezi wa huu kwenye tasnia ya movi za kitanzania yenye aina ya mapigano iliyochezwa na wanawake wakiwa ni kama maadui ndani ya filam hii, Ikiwa ni kati ya filam chache ambazo wanawake wanaigiza kama mashupavu katika swala la mapigano, kwa hilo acha penye sifa wapewe sifa kwani inaonyesha ni jinsi gani bongo movi tuna nia ya kupiga hatua kuelekea ngazi ya wenzetu wa nje kwa wanaopenda kuigiza kama wanawake shupavu kama vile Angelina Jolie.
Pamoja na hayo ni wazi kuwa bado hatujajiandaa kufikia ngazi hiyo ingawaje tunajaribu, lakini tutajaribu mpaka lini wakati tunatakiwa kuongeza juhudi, ujuzi na ufundi ambavyo ndio vitu vikubwa vinavyoiangusha tasnia hii ya filam Tanzania.
Ukiangalia kwa upande wa filam hii ya "We are 4" inajidhihilisha wazi kuwa bado hatuna teknolojia ya kutosha hata kutengenezea sauti maana sauti ilikuwa ikikata yaani maneno hayasikiki lakini ile sauti ya kibwagizo inasikika (Sound track) kwamaana kwamba mafundi mitambo walikuwa wapi muda huo?
Hata tukisema kuwa ni matatizo ya kiufundi lakini bado tatizo linarudi kwa wahusika kwa kushindwa kuitendea haki filamu hii, sawa hatuna vifaa vyenye ubora inamaana ndo hata nakuigiza pia tushindwe jamani?
Kama mmeamua kuigiza kama magaidi kuweni magaidi basi sio ilimradi filamu itaenda sokoni swali ni je inahadhi na ubora wa kuwepo sokoni? kama tumeamua kupiga hatua tupigeni hatua, wenzetu nje wanafanyia filam maandalizi mwaka mzima watu wanajifunza, wanafanya mazoezi ya ngumi, wengine kama ni wanene wanafanya mazoezi ya kupunguza mwili ili aendane na filamu inavyomtaka aigize laiti kama Angelina Jolie angekuwa hafanyi mazoezi yanayotakiwa asingefikia pale alipo kwa sasa na kama wanawake wanataka kuigiza filamu za aina ya mapigano basi |Angelina ndio mfano mzuri.
Kwa mfano ndani ya filam hii kuna kipande ambacho Kamanda wa polisi Abdi (Khalifan Ahmad) alikuwa amekaa sebuleni anawaza mke wake akamuuliza anawaza nini? akamjibu kuwa amepokea simu kuwa kuna mauaji yametokea lakini ukimuangalia askari mwenyewe kama hana habari vile wataki hiyo ni kesi amabayo ipo chini ya usimamizi wake ukizingatia kitu kama hicho kimetokea unatakiwa uwahi eneo la tukio maana unaweza ukapata kitu chochote ambacho kingeweza kukusaidia katika uchunguzi inamaana hata filamu za wenzetu huwaga hatuangalii ili kujua askari polisi huwa anatakiwa awe vipi pindi linapotokea tukio kama hili?
Kipande kingine ni pale askari polisi walipoenda kulinda nyumba ya shahidi lakini cha kushangaza wote wakakaa getini kwa mana kwamba wanalinda nyumba ama ni geti? tuna nia ya kufahamika kimataifa kweli?
Bongo movie tunaweza cha msingi ni kujitahidi tu kuongeza bidii na kuacha kuigiza tunatakiwa tuigize kitu kinachoendana na kweli kama sivyo tutaishia kwenye filamu za kimapenzi tu na za kichawi.
Stori inahusu wasichana wanne Olivia (Bumi Fred Mwakapala), Flaviana (Bukab Fred Mwakapala), Revina (Elberlin Elyud) ambao walikuwa wakifanya shughuli za kijambazi ikiwemo kuiba magari chini ya uongozi wa Big Dada(Fatyhia Chijumba) ambae ndiye aliyekuwa akiwatumikisha madada hao, Vita vilianza pale tu walipoenda kuiba madini kwenye Kampuni mmoja iliyokuwa ikijihusisha na madini na wakasababisha mauaji ya boss wa kampuni hiyo, kwa bahati mbaya msaidizi akafanikiwa kuwatambua na ndipo msako ulipoanza na hatimaye wakauwawa na askari polisi kwenye mashambulizi hayo.
Washiriki: Khalifan Ahmad, Fatyhia Chijumba, Bumi Fred Mwakapala, Bukab Fred Mwakapala, Elberlin Elyud
Aina ya Filam: Mapigano
Ilitolewa: 18/09/2014
Sunday, September 21, 2014
KWA MTINDO HUU BONGO MOVIE HATUTAFIKA
Chausiku ni kati ya filam mpya zinazofanya vizuri katika tasnia ya bongo movie zilizotoka ivi karibuni kwani ina stori nzuri ya kusisimua na washirika wamevaa vizuri ushirika wao haswa mwanadada Shemsa Ford.
Kwa kawaida tumezoea kuwa Chausiku ni jina la mtoto wa kike halikadhalika filam hiyo inavyomzungumzia msichana huyo Chausiku (Shemsa Ford), lakini cha kushangaza ni pale kava la filam anapotawala mtu tofauti ambaye siye muhusika mkuu wa filama hiyo na ukiangalia katika kava la filam hii sehemu kubwa imetawaliwa na mvulana vile vile hata kwa kuangalia unashindwa kumtambua muhusika mkuu ni yupi.

Hivyo waaandaaji bado wanahitaji kujifunza kutengeneza kava kulingana na stori pamoja na muhusika mwenyewe ili kutowachanganya wanunuaji wa filamu.
Stori inamuhusu msichana mjinga Chausiku (Shamsa Ford) anayeishi maisha ya hali ya chini (Uswahilini) ambayo yanampelekea kuwa mtukutu, anaependa ugomvi na kukosa ustaarabu na heshima, pamoja na hayo Dickson (Rammy Galis) anatokea kumpenda ambaye ni mvulana wa kitajiri kitu ambacho kina wakera sana wazazi wake ukizingatia walishamchagulia mchumba wa kuoa ambaye ni msichana wa kitajiri Grace (Hamisa Mobeto) na kusababisha kutoelewana kati ya Dickson na wazazi wake, Hivyo kuamua kujaribu kubadilisha mfuma wa maisha anayoishi Chausiku bila mafanikio, Mwisho wa yote wanafanikiwa kufunga ndoa huku Dickson na wazazi wake kukubaliana na hali halisi ya maisha ya Chausiku.
Casts: Shamsa Ford, Rammy Galis, Hamisa Mobeto, Haji Adam, Mayasa Mrisho, Cathy Rupia.
Genres: Comedy, Family conflict, Drama
Released: 11th September, 2014
Subscribe to:
Comments (Atom)