Sunday, October 19, 2014

MUZIKI WA BONGO UPO JUU KULIKO FILAMU

Ni wazi kuwa soko la muziki linakuwa kwa kasi sana kuliko soko la  filamu kwa upande wa Tanzania kwani hata katika upande wa ubora pia wapo juu kuliko upande wa filamu.

Sasa sijui ni ubahili wa wandaaji ama inakuaje, na kama ni ubahili hii kasumba itaisha lini wakati huu ndo muda wa kutambulisha soko letu kitaifa kutokana na utandawazi kama upande wa muziki wanavyofanya sio siri wasanii wa muziki wanajitahidi katika swala la kuitambulisha Tanzania kimataifa tofauti na upande wa filamu maana tangu Kanumba afariki sijawahi ona filamu iliyoigizwa kwa kushirikisha wasanii wa nje kama alivyokuwa akifanya marehemu Kanumba (The Great)

Tulizani kuwa kifo chake ndo kingekuwa ni changamoto kwa waigizaji wakubwa kama Vicent Kigosi (Ray) kuendeleza pale alipoachia marehemu lakini matokeo yake filamu nyingi zinakuwa katika mfumo wa vichekesho ambapo ndipo wasanii wengi wanapokimbilia siku izi kwasababu hazina garama sana, kwa mtindo huu tutaendelea kweli?

Sio siri filamu za kitanzania huwa zinatia uvivu sana kutizama hasa kwa wale wenye elimu ya juu tena ndo huwaga hawataki hata kuzisikia kabisa, na ndio maana hatuendelei kwasababu sisi wenyewe kama watanzania tunashindwa kuchangia soko hili la filamu kwasababu hazina ubora, kwanini tusitumie pesa nyingi katika kutengeneza filamu ili badae ilete faida zaidi? kwani mataifa mengine wameweza wananini mpaka watanzania tushinde?

Waandaji achene ubahili ili kutengeneza kazi iliyo bora kama wasanii wakubwa wanavyofanya kama  Diamond, Linah na Ommy Dimpoz.

No comments:

Post a Comment