Tuesday, September 30, 2014

BONGO MOVIE KUFIKIA NGAZI YA HOLLYWOOD HATUA BADO NI NDEFU SANA


"We are 4" (Tupo wanne) ni kati ya filamu mpya  zilizotoka ndani ya mwezi wa huu kwenye tasnia ya movi za kitanzania yenye aina ya mapigano iliyochezwa na wanawake wakiwa ni kama maadui ndani ya filam hii, Ikiwa ni kati ya filam chache ambazo wanawake wanaigiza kama mashupavu katika swala la mapigano, kwa hilo acha penye sifa wapewe sifa kwani inaonyesha ni jinsi gani bongo movi  tuna nia ya kupiga hatua kuelekea ngazi ya wenzetu wa nje kwa wanaopenda kuigiza kama wanawake shupavu kama vile Angelina Jolie.

Pamoja na hayo ni wazi kuwa bado hatujajiandaa kufikia ngazi hiyo ingawaje tunajaribu, lakini tutajaribu mpaka lini wakati tunatakiwa kuongeza juhudi, ujuzi na ufundi ambavyo ndio vitu vikubwa vinavyoiangusha tasnia hii ya filam Tanzania.

Ukiangalia kwa upande wa filam hii ya "We are 4" inajidhihilisha wazi kuwa bado hatuna teknolojia ya kutosha hata kutengenezea sauti maana sauti ilikuwa ikikata yaani maneno hayasikiki lakini ile sauti ya kibwagizo inasikika (Sound track) kwamaana kwamba mafundi mitambo walikuwa wapi muda huo?

Hata tukisema kuwa ni matatizo ya kiufundi lakini bado tatizo linarudi kwa wahusika kwa kushindwa kuitendea haki filamu hii, sawa hatuna vifaa  vyenye ubora inamaana ndo hata nakuigiza pia tushindwe jamani?

Kama mmeamua kuigiza kama magaidi kuweni magaidi basi sio ilimradi filamu itaenda sokoni swali ni je inahadhi na ubora wa kuwepo sokoni? kama tumeamua kupiga hatua tupigeni hatua, wenzetu nje wanafanyia filam maandalizi mwaka mzima watu wanajifunza, wanafanya mazoezi ya ngumi, wengine kama ni wanene wanafanya mazoezi ya kupunguza mwili ili aendane na filamu inavyomtaka aigize laiti kama Angelina Jolie angekuwa hafanyi mazoezi yanayotakiwa asingefikia pale alipo kwa sasa na kama wanawake wanataka kuigiza filamu za aina ya mapigano basi |Angelina ndio mfano mzuri.

Kwa mfano ndani ya filam hii kuna kipande ambacho Kamanda wa polisi Abdi (Khalifan Ahmad) alikuwa amekaa sebuleni anawaza mke wake akamuuliza anawaza nini? akamjibu kuwa amepokea simu kuwa kuna mauaji yametokea lakini ukimuangalia askari mwenyewe kama hana habari vile wataki hiyo ni kesi amabayo ipo chini ya usimamizi wake ukizingatia kitu kama hicho kimetokea unatakiwa uwahi eneo la tukio maana unaweza ukapata kitu chochote ambacho kingeweza kukusaidia katika uchunguzi inamaana hata filamu za wenzetu huwaga hatuangalii ili kujua askari polisi huwa anatakiwa awe vipi pindi linapotokea tukio kama hili?

Kipande kingine ni pale askari polisi walipoenda kulinda nyumba ya shahidi lakini cha kushangaza wote wakakaa getini kwa mana kwamba wanalinda nyumba ama ni geti?  tuna nia ya kufahamika kimataifa kweli?

Bongo movie tunaweza cha msingi ni kujitahidi tu kuongeza bidii na kuacha kuigiza tunatakiwa tuigize kitu kinachoendana na  kweli kama sivyo tutaishia kwenye filamu za kimapenzi tu na za kichawi.




Stori inahusu wasichana wanne Olivia (Bumi Fred Mwakapala), Flaviana (Bukab Fred Mwakapala), Revina (Elberlin Elyud) ambao walikuwa wakifanya shughuli za kijambazi ikiwemo kuiba magari chini ya uongozi wa Big Dada(Fatyhia Chijumba) ambae ndiye aliyekuwa akiwatumikisha madada hao, Vita vilianza pale tu walipoenda kuiba madini kwenye Kampuni mmoja iliyokuwa ikijihusisha na madini na wakasababisha mauaji ya boss wa kampuni hiyo, kwa bahati mbaya msaidizi  akafanikiwa kuwatambua na ndipo msako ulipoanza na hatimaye wakauwawa na askari polisi kwenye mashambulizi hayo.



Washiriki: Khalifan Ahmad, Fatyhia Chijumba, Bumi Fred Mwakapala, Bukab Fred Mwakapala, Elberlin Elyud
Aina ya Filam: Mapigano
Ilitolewa: 18/09/2014

 

No comments:

Post a Comment