Sunday, September 21, 2014

KWA MTINDO HUU BONGO MOVIE HATUTAFIKA

Chausiku ni kati ya filam mpya zinazofanya vizuri katika tasnia ya bongo movie zilizotoka ivi karibuni kwani ina stori nzuri ya kusisimua na washirika wamevaa vizuri ushirika wao haswa mwanadada Shemsa Ford.
Kwa kawaida tumezoea kuwa Chausiku ni jina la mtoto wa kike halikadhalika filam hiyo inavyomzungumzia msichana huyo Chausiku (Shemsa Ford), lakini cha kushangaza ni pale kava la filam anapotawala  mtu tofauti ambaye siye muhusika mkuu wa filama hiyo na ukiangalia katika  kava la filam hii sehemu kubwa imetawaliwa na mvulana vile vile hata kwa kuangalia unashindwa kumtambua muhusika mkuu ni yupi.
Hivyo waaandaaji bado wanahitaji kujifunza kutengeneza kava kulingana na stori pamoja na muhusika mwenyewe ili kutowachanganya wanunuaji wa filamu.


Stori inamuhusu msichana mjinga Chausiku (Shamsa Ford) anayeishi maisha ya hali ya chini (Uswahilini) ambayo yanampelekea kuwa mtukutu, anaependa ugomvi na kukosa ustaarabu na heshima, pamoja na hayo Dickson (Rammy Galis) anatokea kumpenda ambaye ni mvulana wa kitajiri kitu ambacho kina wakera sana wazazi wake ukizingatia walishamchagulia mchumba wa kuoa ambaye ni msichana wa kitajiri Grace (Hamisa Mobeto) na kusababisha kutoelewana kati ya Dickson na wazazi wake, Hivyo kuamua kujaribu kubadilisha mfuma wa maisha anayoishi Chausiku bila mafanikio, Mwisho wa yote wanafanikiwa kufunga ndoa huku Dickson na wazazi wake kukubaliana na hali halisi ya maisha ya Chausiku.

Casts:  Shamsa Ford, Rammy Galis, Hamisa Mobeto, Haji Adam, Mayasa Mrisho, Cathy Rupia.
Genres: Comedy, Family conflict, Drama
Released: 11th September, 2014

No comments:

Post a Comment