Nendeze ni kati ya filamu ya kitanzania inayofanya vizuri katika tasnia hii ya filam ikiwa ni muendelezo wa filam ya mwali wa kizaramo.
Sio siri penye sifa acha wapewe sifa kiukweli wamejitahidi kwenye uandaji wa filam hii haswa kwa upande wa mapigano (action) ukizingatia ni wasanii wachanga ambao ndio kwanza wanaanza lakini wamefanya mambo mazuri sana kwani hata katika upangaji wa ngumi wamepanga vizuri halikadhalika pia washiriki wameshiriki vyema kwa inaonesha ni wazi kuwa walifanyia mazoezi ya kutosha sana tofauti na tulizoea kuona mambo hayo yakifanywa na wasanii wakubwa kama kina Bad Boy, na Seba.
Tofauti na wasanii wengine wamezoea kushirikisha wasanii wakubwa ili kutoka kisanaa, lakini ni kitu cha kufurahisha sana kuona kuwa kuna vipaji vikubwa nyuma ya pazia mbali na kina Vicent Kigosi, Jacob Stephen, Hemedi Suleiman ambao ndio wamezoeleka kama mtu ukitaka kuuza filam zao kazi yako na kama tukiendelea kutoa kazi nzuri kama hizi basi tutafika mbali, ingawaje ni filamu ambazo hazina soko kubwa sana kwasababu bado ni wasanii wachanga.
Pamoja na hayo bado kuna kasumba ya kuwa ili mtu ujulikane ama uonekane kuwa ni ni jambazi ama una mabavu ni lazima atavaa koti kubwa na anakuwa anatembea kwa kujitanua sana hata sijui ni kwanini na ndo tumeshazoea kwanini wasiwe tu wanaonekana kawaida kwani ili mtu kuwa jambazi si lazima utumie nguvu kwani hata akili tu inatosha lakini hilo ni swala gumu kwa watanzania, ingekuwa ni bora zaidi kama wangejaribu kucheza filamu ambazo wanatumia akili zaidi kwani filam nyingi za kibongo mtu ukitizama unakuwa unajua kabisa mwisho wake utakuaje na story nyingi zinakuwa zikijirudia.
Stori inamuhusu Nendeze(Latifa Shabani) ambae alitokea kumpenda kijana Mashaka ( na kukataa kuolewa na kijana wa kitajili Mr.Karan (Hashim Rajab Dituth) ambae alipendekezwa na wazazi wake kitendo amnbacho kinachosababisha vita na familia kumtenga kwa kuwa alikiuka matakwa ya familia yake,pamoja na hayo Mudi(Mohamed Salum) ambae ni kaka wa Nendeze alikuwa akipinga mapenzi ya mashaka na Nendeze hakuridhika kuwaona wakiwa pamoja hivyo kuchoma nyumba yao moto, lakini Nendeze na Mashaka walifanikiwa kujiokoa kwenye moto huo na kwenda kujificha porini ndipo wanakijiji walipoamua kujiunga na kuwatafuta na ndipo vita kati ya kikosi cha Mudi na Wanakijiji lakini mpaka mwisho wa siku walifanikiwa kushinda na kuendelea kuishi vizuri na familia zao.
Aina ya Filam:Migogoro ya Kifamilia, Mapigano
washiriki: Mohamed Salum, Latifa Shabani, Halima Hashim, Hashim Rajab Dituth.
No comments:
Post a Comment